Numbers 26:5-10

5 aWazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa: kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki;
kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;

6 bkutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;
kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.

7Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.

8Mwana wa Palu alikuwa Eliabu, 9 cnao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Musa na Haruni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana. 10 dArdhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo.
Copyright information for SwhKC